Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imewapa siku 30 wataalamu wenye madeni ya ada za mwaka za usajili kulipa madeni hayo, ikionya kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Godfred B. Mbanyi, kupitia tangazo la Bodi, akiwataka wataalamu ambao hawajakamilisha malipo ya ada zao kuhakikisha wanatimiza wajibu huo ndani ya muda uliowekwa.
Mbanyi amesema wataalamu watakaoshindwa kulipa madeni yao ndani ya siku 30 wanaweza kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bodi, ikiwamo hatua zinazohusiana na usajili wao.
"PSPTB imepewa mamlaka chini ya Sheria ya PSPTB, Sura ya 179 ya Sheria za Tanzania, kusimamia na kudhibiti taaluma ya ununuzi na ugavi nchini, ikiwa ni pamoja na usajili wa wataalamu, " Amesema Mkurugenzi Mtendaji Mbanyi
Na Kuongeza kuwa "Wataalamu wenye madeni wanapaswa kutumia muda huo kuhakikisha wanakamilisha malipo yao ili kuepuka hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yao baada ya muda huo kuisha, " Amesema Mbanyi.
Aidha, PSPTB imeonya kuwa kushindwa kutekeleza agizo hilo kunaweza kuhusisha hatua za kiutawala na kisheria kwa mujibu wa taratibu za Bodi, huku taarifa za utekelezaji zikitolewa kupitia njia rasmi.
Aidha amesema Majina ya wataalamu wote waliokamilisha malipo yao na wasio na madeni yatachapishwa kwenye Gazeti la Serikali pamoja na tovuti rasmi ya PSPTB.
"Kwa mtaalamu yeyote ambaye jina lake halitaonekana kwenye orodha hiyo anatakiwa kutambua kuwa amefutwa kwenye daftari la usajili kutokana na migogoro ya madeni, " Amesema
na Kuongeza "Lengo kuu la hatua hii ni kuzuia kuingizwa kwa taarifa zisizo sahihi au "data chafu" kwenye mfumo mpya wa usajili unaojengwa sasa. PSPTB imewasihi wataalamu wote kujitokeza kwa wakati na kulipa ada zao ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza katika shughuli zao za kitaalamu, " Amesema Mkurugenzi Mtendaji huyo

.jpeg)





0 Comments