Header Ads Widget

KUWASA YAANZA KUFUNGA MITA ZA MALIPO YA AWALI KWA WATEJA WAKE.

‎Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma Ujiji imeanza kutekeleza mpango wa kufunga dira za maji za maalipo ya awali (Prepaid) ambapo katika awamu ya kwanza mpango huo unatarajia kufikia wateja 100 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma Ujiji (KUWASA), Dk.Christopher Nditi alisema hayo wakati kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2026, Wazo Mwang’onda akizindua uwekaji na ugawaji wa mita hizo kwa wateja wa manispaa hiyo ambapo alisema kuwa katika hatua ya awali wateja  80 wameshafungiwa mita hizo na wateja wengine  20 mchakato wa kuwafungia unaendelea.

Dk.Nditi alisema kuwa wakati mchakati unaendelea kukamilisha kufunga dira hizo kwa wateja 100 tayari katika mpango wa muda mfupi Mamlaka imeshaweka oda ya ununuzi wa mita nyingine 1500 alisema ili kuhakikisha wateja Zaidi wanaingia kwenye utaratibu huo.

Sambamba na hilo alisema kuwa mamlaka hiyo katika mpango wa muda mrefu inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 11 kutekeleza mradi wa kufunga mita za maji za malipo ya awali (Pre Paid) kwa wateja 28,000 wa manispaa ya Kigoma Ujiji na vitongoji vyake ili kuwezesha wananchi kujikadiria matumizi ya huduma hiyo katika maeneo yao.

 Mkurugenzi huyo alisema kuwa ufungaji wa mita hizo ni sehemu ya mpango mkakati wa mamlaka hiyo wa kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana karibu na wananchi lakini pia wananchi kutumia huduma hiyo kulingana na gharama wanayojipangia na hiyo itaondoa malalamiko ya wateja kubambikiwa bili.

Akizungumza kabla ya kuzindua mpango huo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2026, Wazo Mwang’onda ameitaka mamlaka hiyo kutekeleza mradi huo kulingana na mpango ulkioelezwa kwani inaonekana utatatua changamoto nyingi za maji hasa suala la malipo kutokana na wananchi kulalamika kupewa bili kubwa ambayo hailingani na gharama.

 Mwang’onda alisema kuwa ufungaji wa mita hizo uende sambamba na upatikanaji wa uhakika wa huduma za maji safi na salama ambapo alibainisha kuwa taarifa alizopata na video inayoeleza shughuli mbalimbali za mamlka hiyo alizooona anaamini yanayosemwa yatatimizwana siyo taarifa kwa ajili ya mwenge pekee hivyo mpango huo uwezesha wananchi kutumia muda mwingi kwa shughuli za maendeleo badala ya kutafuta maji.

 Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua alisema kuwa serikali ya wilaya imekuwa ikisimamia kwa karibu utendaji wa mamlaka hiyo hasa kuhakikisha huduma ya maji safi na salama yanapatikana kwa wananchi lakini pia suala la changamoto za bili kubwa za maji kwa wateja wamekuwa wakilishughulikia kwa kiwango kikubwa na ndiyo yaliyozaa mpango huo wa mita za malipo ya awali.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI