Header Ads Widget

MBUNGE ACT AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MIRADI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kaskazini kwa Chama cha ACT Wazalendo Kiza Nayeye  na wananchi wa kata ya Simbo Halmashauri ya wilaya Kigoma wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa miradi mikubwa iliyoletwa kwenye maeneo yao ambayo imeondoa changamoto kubwa zilizokuwa zikikabilia maisha yao ya kila siku.

Wananchi hao wamesema hayo wakati mwenge wa uhuru ukiweka mawe ya msingi katika miradi ya ujenzi wa shulee mpya ya sekondari ya Msimba Day na madaraja 16 ya mawe miradi ambayo ilikuwa kero kubwa kwa wananchi haao na kikwazo katika mipango yao mbalimbali ya maendeleo.

Wa kwanza kutoa shukrani hizo alikuwa mbunge Kiza Mayeye ambaye alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo ilikuwa changamoto kubwa kwa wananchi wa kata hiyo ambao walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za shule ya Sekondari katika shule ya Mwandiga.

Wakieleza adha ya ukosefu wa shule ya sekondari katika kata yao wananchi hao akiwemo Hussna Omari ambaye alisema kuwa kutembea umbali mrefu kulikuwa na athari kubwa kwa wanafunzi na wazazi maana kama siyo kutembea umbali mrefu basi  inabidi wazazi kuweka bajeti ya usafiri kila siku hali ambayo wazazi wengi hawakuwa wanamudu.

Naye  Charles Francis Mkazi wa kijiji cha Msimba alisema kuwa changamoto ya shule kuwa mbali ilikuwa na athari nyingi kwa wanafunzi na wazazi hivyo baadhi ya familia ambazo zilikuwa hazizingatii umuhimu wa elimu watoto wengi walikuwa wanakatisha masomo.

Kufuatia ujenzi wa shule hiyo Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Wazo Mwang’onda alitoa rai kwa wazazi kutumia utekelezwaji wa mradi huo kama jambo la thamani kwao kwa kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule, wanazingatia masomo lakini pia kuhakikishaa miradi hiyo inalindwa na kutunzwa ili kuwanufaisha wananchi wengi kwa kipindi kirefu.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kigoma,Chiriku Chilumba alisema kuwa shule hiyo itakayogharimu kiasi cha shilingi milioni 603 ni moja kati ya shule mbili zilizojengwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi lakini pia kujiandaa na ongezeko kubwa la wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka ujao ambapo wanafunzi wa darasa la saba na darasa la sita wanaomaliza mwaka huu kwa pamoja wataanza kidato cha kwanza mwaka ujao.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI