Na. Matukio Daima, Geita
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeeleza namna tafiti na huduma zake za kitaalamu zinavyoweza kuwa nyenzo muhimu kwa wachimbaji na wawekezaji katika kuongeza ufanisi wa shughuli za uchimbaji madini nchini.
Akizungumza katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Samia Suluhu Hassan mkoani Geita, Afisa Masoko wa GST, Jeremia Mgale, amesema taasisi hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo ramani za kijiolojia, uchunguzi wa miamba, upimaji wa kemia ya udongo pamoja na taarifa kuhusu maeneo yenye viashiria vya madini.Amesema huduma hizo zinamwezesha mchimbaji kupata uelewa wa aina ya madini yanayopatikana katika eneo husika, pamoja na kufahamu mbinu na teknolojia zinazofaa katika uchimbaji, badala ya kufanya shughuli hizo kwa kubahatisha.
Kwa upande wake, Mjiolojia kutoka GST, Andrew Bulusa, amesema taasisi hiyo imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali za kijiosayansi, uchunguzi wa madini na uchambuzi wa sampuli kwa ajili ya kutoa taarifa sahihi zinazoweza kutumiwa na wadau wa sekta hiyo.
Bulusa amesema GST pia hutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau wanaohusika na shughuli za madini, ujenzi na mazingira, hatua ambayo inasaidia kuongeza uelewa na matumizi sahihi ya taarifa za kitaalamu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Amesema tafiti na taarifa zinazotolewa na GST zina umuhimu mkubwa katika kuchochea uwekezaji kwenye sekta ya madini na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi na pato la Taifa.
Aidha, amewataka wananchi, wachimbaji na wawekezaji wanaoshiriki maonesho hayo kutembelea banda la GST ili kupata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo, pamoja na kupata ramani na taarifa mbalimbali za kitaalamu zinazoweza kuwasaidia katika shughuli zao.
MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA
MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️
1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA
PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM
PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
3:TUZO YA AFYA
PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
4:TUZO YA MPIGA PICHA
PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA
AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .







0 Comments