Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanaimarisha uongozi unaoendelea ili kuongeza chachu ya maendeleo ndani ya Chama, Jumuiya hiyo na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Kikwete ameyasema hayo, Septemba 26, 2026 wakati wa Baraza la Jumuiya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Kikwete uliopo Halmashauri ya Chalinze.
Amesema endapo kuna kiongozi ambaye hafai katika nafasi yake, anapaswa kuwekwa kando akisisitiza kuwa siri kubwa ya mafanikio katika eneo lolote ni kuwa na uongozi bora, endelevu na wenye maono ya maendeleo.
Mhe. Kikwete amesema dhamira ya CCM, Jumuiya ya Wazazi na Serikali kwa ujumla ni kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika jamii.
Amesema kama ilivyo mzazi ambaye anatamani kuona mtoto wake akipata maendeleo, Jumuiya ya Wazazi ina wajibu wa kuhakikisha watoto na vijana wanalelewa katika misingi bora ili kujenga kizazi kitakachoweza kuwa viongozi bora wa baadae.
Aidha, Mhe. Kikwete amempongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Mohamed Mzimba kwa kuendelea kusimamia vyema Jumuiya hiyo ambapo amemtaka Mzimba pamoja na wajumbe wa Baraza hilo kuendelea kukisemea Chama Cha Mapinduzi, utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho pamoja na maendeleo yanayotekelezwa kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo, Mohamed Mzimba amemshukuru Mhe. Kikwete na kumpongeza kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Jumuiya inazidi kuleta heshima ndani ya Wilaya ya Bagamoyo huku akiweka wazi kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya 6 katika Wilaya ya Bagamoyo.
![]() |
| Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo, Mohamed Mzimba |








0 Comments