Header Ads Widget

ASILIMIA 98 YA MANUNUZI YA KAMPUNI YA UCHIMBAJI YAFANYIKA TANZANIA


Na. Matukio Daima Media Geita

Kampuni inayojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini chini ya ardhi kwa kushirikiana na kampuni ya Kitanzania imesema inaendelea kuchangia pato la Taifa kupitia uzalishaji wa madini, huku ikipanua fursa za ajira, biashara na mafunzo kwa Watanzania.

Akizungumza wakati wa Maonyesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita, Afisa wa kampuni hiyo, Saad Simba, alisema kampuni imeweka mkazo katika utekelezaji wa sera ya local content kwa kuhakikisha Watanzania na kampuni za ndani zinapata nafasi ya kushiriki katika shughuli za uchimbaji.

Simba alisema takribani asilimia 98 ya manunuzi ya kampuni hufanyika ndani ya Tanzania, hatua ambayo amesema imeongeza ushiriki wa kampuni za Kitanzania katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na sekta ya madini

“Kwa upande wa local content tunafanya vizuri. Takribani asilimia 98 ya manunuzi yetu yanafanyika ndani ya nchi, lakini pia tumetoa nafasi kwa kampuni za Kitanzania kujifunza na kushiriki katika shughuli zetu,” alisema.


Aidha, alisema kampuni imeanzisha kituo cha mafunzo mjini Geita kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ujuzi wa kuendesha na kutumia mitambo mikubwa inayotumika katika uchimbaji wa madini chini ya ardhi.

Kwa mujibu wa Simba, mafunzo hayo yanalenga kuwapatia vijana ujuzi wa kitaalamu utakaowawezesha kushiriki kikamilifu zaidi katika sekta ya madini na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.

Alisema kampuni hiyo pia inaendelea kushirikiana na Tume ya Madini pamoja na Wizara ya Madini katika shughuli mbalimbali zinazolenga kuendeleza sekta hiyo na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya Taifa.

“Tunashirikiana na Tume ya Madini na Wizara ya Madini katika shughuli mbalimbali za kuchangia maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania,” alisema.

Akizungumzia shughuli za kampuni hiyo nje ya Geita, Simba alisema kampuni mama, Perenti, inaendesha shughuli za uchimbaji katika maeneo mbalimbali, huku ikiendelea kutafuta namna ya kutumia teknolojia na utaalamu unaopatikana nchini katika kukuza sekta ya madini.

Alisema kwa upande wa Tanzania, kampuni inaendelea na mradi wake mmoja, huku ikilenga kuongeza ushiriki wa Watanzania katika shughuli za uchimbaji, teknolojia na huduma mbalimbali zinazohusiana na sekta ya madini.

Kwa ujumla, kampuni hiyo imeeleza kuwa itaendelea kuwekeza katika local content, mafunzo ya vijana, ajira na matumizi ya kampuni za ndani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha sekta ya madini inatoa fursa zaidi kwa Watanzania na kuchangia maendeleo ya Taifa.

 

 KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI