Wananchi mkoani Njombe wameitaka bodi mpya ya maji katika mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Njombe mjini NJUWASA Kuanza kutekeleza majukumu yake kwa kuhakikisha wananchi waliokosa kabisa maji wanafikishiwa maji pamoja na kwenda kusikiliza maoni ya changamoto za maji.
Wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo yenye wajumbe 10 ikiongozwa na Ndugu Fidelis Lumato ambaye ameteuliwa kwa awamu nyingine wakazi hao akiwemo Dowson Msumange na Deo Mazao Sanga Diwani wa kata ya Njombe mjini wamesema wanatarajia kuona bodi hiyo mpya itakwenda kuwa suluhu ya changamoto ya maji hasa kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji pamoja na kuwafikishia huduma ambao hawajapata kabisa.
Awali mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira njombe mjini Njuwasa Mhandisi Robert Lupoja amesema hadi sasa kuna upungufu wa maji Takribani lita milioni tano kwa siku jambo ambalo wanaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake Eunice Lwendo amesema bodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya utendaji wake imefanikiwa kusimamia mamlaka hiyo kwa uadilifu mkubwa na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji huku wakishauri bodi mpya kwenda kusimamia utekelezaji wa miradi walioiacha.
Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe,Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Zakaria Mwansasu ameiagiza bodi hiyo mpya ya wakurugenzi kuanza kazi haraka kwa kutembelea vyanzo vya maji na kuanza kuchukua hatua dhidi ya taarifa za ujio wa mvua za El nino.


.jpeg)





0 Comments