Ngorongoro: Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) imetangaza kuuawa kwa simba kumi (10) katika eneo la Ndutu, Kata ya Endulen.
Tukio hilo limetokea Septemba 18, 2026, na uchunguzi wa awali unaonyesha simba hao wamekula sumu.
Taarifa iliyotolewa Septemba 19 na Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma wa NCAA, Hamis Dambaya, imesema mamlaka imesikitishwa na tukio hilo na imeanzisha uchunguzi wa kina wa kitaalamu kubaini wahusika.
"Taarifa zaidi zitatolewa mara uchunguzi utakapokamilika," imesema NCAA.






0 Comments