Header Ads Widget

WANNE KIZIMBANI KWA MAUAJI Y A RAIA WA CHINA

 



Matukio Daima, Dar 


Watu wanne wamefikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara mwenye asili ya China, Baozhang Ge maarufu kama Lodaa.


Washtakiwa  katika hiyo ni, Godson Simon Paul, Elisha Saitoti Sapayoni Lukumai, Godfrey Laban Mollel na Godson Pintel Lesikar walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Is-haq Kuppa.


Wakili wa Serikali Harrison Lukosi alidai kuwa Mei 16, 2026 katika eneo la Mabibo Sokoni, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam washtakiwa walitenda kosa la mauaji ya kukusudia.




Wakili  Lukosi alidai washtakiwa hao wanadaiwa kumuua kwa makusudi Lodaa, kinyume cha Kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya mwaka 2023.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, tuliomba tarehe ya kutajwa.


Hakimu alisema mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji hivyo washtakiwa hawatakiwi kujibi chochote mpaka pale kesi yao itakapokamilika upelelezi itahamishiwa Mahakama Kuu.


Alisema kesi hiyo itatajwa Julai 23, 2026 na washtakiwa wapelekwe mahabusu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI