Header Ads Widget

REKODI MPYA MLIMA KILIMANJARO MZEE WA MIAKA 90 AKWEA KILELE CHA UHURU



Raia kutoka nchini Marekani daktari mstaafu  Art Ulene, ameandika historia mpya baada ya kufanikiwa kufika katika Kilele cha Uhuru, Mlima Kilimanjaro, na kuvunja rekodi ya kuwa miongoni mwa watu wenye umri mkubwa zaidi kufikia kilele hicho jana Julai 13, 2026. Mafanikio hayo yameambatana na sherehe ya kipekee ya kukata keki juu ya kilele ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.

Katika tukio hilo Dkt. Ulene alikata keki akiwa amezungukwa na waongoza watalii, wapagazi, na wapandaji wenzake huku wakimpongeza kwa ujasiri, wakimtakia afya njema na pamoja na kumpongeza kwa adhma yake ya kutimiza ndoto hiyo katika umri wa miaka 90.

Mafanikio hayo yameendelea kuitangaza Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla kama kitovu cha utalii wa milima duniani, yakionyesha uwezo wa Mlima Kilimanjaro kuwavutia wageni wa rika mbalimbali wanaotafuta changamoto, mafanikio binafsi na mandhari ya kipekee.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI