Header Ads Widget

RAIS DKT. MWINYI: TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIF

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Tamko la Pamoja kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo linafungua njia ya utekelezaji wa uundaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuimarisha amani, umoja, mshikamano na maendeleo ya Zanzibar.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa ajenda zilizokubaliwa kwa pande zote mbili kwa ajili ya kufanyiwa kazi kufuatia Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa Zanzibar baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo tarehe 09 Julai, 2026.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema maridhiano hayo yanaonesha dhamira ya viongozi kuweka mbele maslahi ya taifa, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha mchakato huo unadumisha utulivu, utawala bora na maendeleo endelevu.


Halikadhalika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongeza hatua hiyo akieleza kuwa maridhiano hayo yanafungua ukurasa mpya wa kuimarisha umoja, utulivu na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari, na ni ishara ya ukomavu wa kisiasa na dhamira ya kujenga mazingira ya amani na maendeleo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Mhe. Othman Masoud Othman, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kuendeleza mchakato wa maridhiano, akisema umefungua njia ya kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu wa changamoto za kisiasa Zanzibar.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi; Marais Wastaafu wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume na Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein; Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla; Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa dini, Viongozi wa Serikali za SMT na SMZ, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mabalozi, Wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa pamoja na wananchi mbalimbali.

















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI