Header Ads Widget

JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MGANGA KWA MAUAJI YA WATU WANNE


HAI.

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja aitwaye Beatrice Urassa (59) kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne ambao walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Machame Wilayani Hai.

Akithibitisha kukamatwa kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, SACP Saimon Maigwa aliwataja waliofariki dunia ni Hamida Hamis Kweka (26), Robson Edson Meena (34), Ismail Exaud Uronu (34) na Kamama Exaud Uronu (45) wote wakazi wa kitongoji cha kinyaro, kata ya Mnadani, wilaya ya Hai na Mkoa wa Kilimanjaro.

Kamanda Maigwa alisema kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwapatia dawa za kienyeji watu hao ambao ni ndugu wa familia moja, na kupelekea kufariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu Julai 05 mwaka huu majira ya usiku. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linaendelea na uchunguzi kuhusina na tukio hili, pindi utakapokamilika taratibu nyingine za kisheria zitafuata.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI