Matukio DaimaMedia
Mbunge wa Mkoa wa Kigoma Mjini Revocatus Chipando (Baba Levo) wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora–Kigoma, itakayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo mradi huo utabadilisha sura ya uchumi wa mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,amesema tukio hilo litawakutanisha wananchi pamoja na wasanii mbalimbali wenye asili ya Kigoma na marafiki wa mkoa huo ili kushuhudia uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.
Aidha, amewataja wasanii waliopata mwaliko kuwa ni Ali Kiba, Diamond Platnumz, Linex, Chino wanamani, Dee Voice na Shilole, akisema uwepo wao utatoa hamasa kwa wananchi kushiriki tukio hilo la kihistoria.
Baba levo amesema ameandaa usafiri wa basi kwa baadhi ya wananchi wanaotaka kwenda Kigoma kushiriki hafla hiyo, huku akieleza kuwa utaratibu wa kupata tiketi utawekwa wazi kwa watakaohitaji.
Amessema mradi wa SGR wa Tabora–Kigoma wenye urefu wa kilometa 502 na thamani ya zaidi ya Sh trilioni 6.23 unatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 15,000 na kuimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zambia.
Amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2030 na utaunganisha moja kwa moja Kigoma na Bandari ya Dar es Salaam, hatua itakayorahisisha usafirishaji wa mizigo na kuongeza ushindani wa biashara ndani na nje ya nchi.
"Tunataka wananchi wajue kuwa ujenzi unaendelea vizuri. Kigoma haitakuwa tena mwisho wa reli, bali itakuwa kitovu muhimu cha biashara kwa ukanda wa Maziwa Makuu," amesema.






0 Comments