SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limepata fursa ya kuwapokea Wanafunzi pamoja na Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Seoul kilichopo nchini Korea Kusini, leo Julai 14, 2026 katika Ofisi za Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha.
Ugeni huo ulilenga kujifunza kuhusu shughuli mbalimbali za uhifadhi, utalii na mchango wa Shirika katika kushirikiana na jamii kulinda na kutunza maliasili.
Wanafunzi hao wanatarajia kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tarangire na Ziwa Manyara ili kujionea vivutio vya utalii pamoja na kujifunza kwa nadharia namna shughuli za uhifadhi na utalii zinavyofanyika katika hifadhi hizo.
Ugeni huo umepokelewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Dkt. Bakari Mnaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Uhifadhi TANAPA.












0 Comments