Header Ads Widget

WAANDISHI WAANZA KUWASILISHA KAZI TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

 WAANDISHI wa Habari nchini wameanza kuwasilisha kazi zao kwa ajili ya kushindanishwa kwenye Tuzo za Uandishi wa Habari na Makala za Maendeleo (Samia Kalamu Awards) kwa mwaka 2026.

Tuzo hizo zinaandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).

Taarifa ya pamoja iliyosainiwa na Mwenyekiti wa tuzo hizo, Peter Mwasalyanda na Makamu Mwenyekiti, Rose Reuben, imesem hadi kufikia  Juni 15, 2026, jumla ya kazi za kushindanishwa 624 zilikuwa tayari zimewasilishwa kupitia mfumo wa samiaawards.tz kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Amesema uwasilishaji huo ni mwitikio mkubwa wa waandishi wa habari na vyombo vya habari kushiriki katika tuzo hizi.

“Takwimu za kazi zilizowasilishwa zinaonesha kuwa kazi 20 (asilimia 4.8) ziliwasilishwa katika kundi la tuzo za vyombo vya habari, kazi 25 (asilimia 4.0) katika kundi la tuzo maalumu za kitaifa, na kazi 569 (asilimia 91.2) katika makundi ya tuzo za kisekta.

“Aidha, vyombo vya habari mtandaoni vinaongoza kwa uwasilishaji wa kazi za kushindanishwa, ambapo hadi sasa kazi 276, sawa na asilimia 44 ya kazi zote zilizowasilishwa, zimepokelewa kutoka katika kundi hilo.

“Kwa upande wa makundi mengine ya vyombo vya habari, magazeti yamewasilisha kazi 178, sawa na asilimia 29 ya kazi zote zilizopokelewa; televisheni zimewasilisha kazi 102 (asilimia 16); redio zimewasilisha kazi 60 (asilimia 10); huku majarida yakichangia kazi 8 pekee, sawa na asilimia 1 ya kazi zote zilizowasilishwa.

“Mwitikio huu unaakisi kuongezeka kwa matumizi ya majukwaa ya kidijitali katika uzalishaji na usambazaji wa maudhui ya habari za maendeleo pamoja na dhamira ya waandishi wa habari nchini kuendelea kuelimisha, kuhabarisha na kuhamasisha jamii kuhusu maendeleo ya taifa letu,” imesema taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI