Header Ads Widget

UKATILI SHULENI UNACHANGIA UTORO -KISSINGA

 





Na Fadhili Abdallah,Kigoma

UKATILI unaofanywa shuleni kwa wanafunzi unaelezwa kuchangia utoro au wanafunzi kukimbia na kuacha masomo hali ambayo serikali imeshaanza kuchukua hatua ili kuzifanya shule za msingi na sekondari kuwa sehemu salama na kimbilio la watoto wengi.

 

Kaimu Afisa elimu shule za msingi wa manispaa ya kigoma Ujiji, Cornel Kissinga alisema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa ngazi ya Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji na kubainisha kuwa hatua mbalimbali zimeanza kuchukulia kuondoa vitendo vya ukatili vinavyofanywa na walimu ili  kuwafanya watoto wapende elimu.

 

Kissinga alisema kuwa watoto wengi hasa wale wa madarasa ya mitihani wanatumia muda mwingi wakiwa na walimu shuleni hivyo kama shule inakuwa na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na walimu hali hiyo inajenga uadui na kuwafanya watoto kuacha masomo na kwamba tayari mafunzo yamefanyika kwa walimu lakini pia wanafunzi wanafundishwa kujua haki zao na wapi pa kutoa taarifa wanapofanyiwa vitendo hivyo.

  

Akizungumza katika maadhimisho hayo Afisa anayeshughulisha na jamii kutoka Shirika la Tanzania Wote Equality Alliance (TAWE), Storia Raphael alisema kuwa mashirika madogo yanayoshughulika na masuala ya usawa wa kijinsia kupitia mradi wa wezesha Binti yanapaswa kupaza sauti katika kusimamia na kupigania haki za wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao ikiwemo haki ya kupata elimu.

 

Storia alisema  kuwa Shirika la TAWEA limewezesha masirika saba kushirikia maadhimisho hayo ili kuweza kueleza na kutangaza shughuli zao kwa jamii ili kupanua wigo katika kusimamia haki za wasichana na wanawake.

 

Akihitimisha maadhimisho hayo Katibu Tawala wa wilaya Kigoma,Mganwa Nzota ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya Kigoma,Rashid chuachua alisema kuwa serikali imeendelea kusimamia haki za mtoto na haki hizo zimetambuliwa rasmi kisheria na kuonya yeyote anayekiuka haki hizo anapaswa kuchukuliwa hatua.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI