Header Ads Widget

RC KHERI APONGEZA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA IRINGA

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James  ameipongeza Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani humo kwa kuendelea kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi, akisema hatua hiyo imechangia kuongezeka kwa mapato ya serikali na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),iliyowakutanisha wafanyabiashara na viongozi wa TRA, Kheri James  alisema ulipaji wa kodi ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa, huku akiwahimiza wafanyabiashara kuendelea kuwa waaminifu katika kutekeleza wajibu huo.

Alisema serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na utoaji wa huduma kupitia TRA kwa kupunguza urasimu, kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali na kujenga ushirikiano mzuri na walipakodi ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.

“Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa kodi, bado kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati”alisema

Alisema TRA imeendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa walipakodi kwa kuondoa urasimu, kuimarisha mahusiano na wadau pamoja na kujenga mazingira yanayowezesha ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi.

Aidha, alieleza kuwa ongezeko la makusanyo ya kodi limeiwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo uwanja wa ndege, jingo la utawala,barabara ya Iringa Masembe, miradi mikubwa ya elimu, afya ,maji na miradi mingi inatelekezeka kwa sababu wanazo fedha za kusukuma miradi hiyo.

“Hivyo basi nawahimiza wananchi kuendelea kutimiza wajibu wenu wa kulipa kodi kwa wakati, ushirikiano kati ya serikali, walipakodi na wadau wengine ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo ya nchi”alisema


Kwa upnade wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Iringa Peter Mtalo alimuhaidi Mkuu wa Mkoa kuwa wafanya baiashara wataungana kwa pamoja kuijenga Iringa.

“Nakuahidi mkuu wa mkoa nitaendelea kushirikiana na wenzangu kuwaongoza wafanyabiashara wote kwa ajili ya kuifanya Iringa yetu ing’are, nazingatia ushauri wako kwa Meneja wetu mpya tutampa ushirikiano kadri inavyowezekana nay eye tunaomba awe tayari kushirikiana na wafanyabiashara”alisema Mtalo


Mtalo alitumia nafasi hiyo pia kuipongeza timu ya TRA mkoa wa Iringa kwa kufganya kazi na wafanyabiashara katika hali ngumu lengo ni kujengana na kuijenga Iringa kwa sababu kulipa kodi ndio kulijenga taifa lao. 

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI