Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada kutoka CRDB Bank unaolenga kuboresha afya na ustawi wa watoto watano waliozaliwa hospitalini hapo, ambapo kila mtoto amefunguliwa akaunti yenye TZS 1.5 Mil. na kuwekewa hisa za awali za shilingi laki tano pamoja na bima ya afya ya miaka mitatu kama msingi wa maisha yao ya baadaye.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Delilah Kimambo amesema benki hiyo imeona umuhimu wa kuchukua hatua hiyo kama sehemu ya mchango wake katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto nchini.
Katika hatua nyingine, benki hiyo imemfungulia mama wa watoto hao akaunti yenye thamani ya TZS 4 Mil. ili kumsaidia kujipatia kipato na kuimarisha maisha ya familia, huku baba wa familia akikabidhiwa bajaji mpya kwa ajili ya shughuli za uzalishaji na kuinua ustawi wa familia hiyo kwa ujumla.



















0 Comments