Header Ads Widget

BALOZI WA TANZANIA NCHIN UINGEREZA NDUGU MBELWA KAIRUKI AKUTANA SPIKA WA BUNGE


Tarehe 18 Juni 2026, Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Ndugu Mbelwa Kairuki, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Uingereza Mheshimiwa Sir Lindsay Hoyle katika Makazi Rasmi ya Spika.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Uingereza, hususan katika nyanja za elimu, biashara, uwekezaji, sayansi na teknolojia, pamoja na kuendeleza ushirikiano wa kibunge kati ya nchi hizo mbili.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Kairuki alimweleza Mheshimiwa Spika kuhusu maandalizi ya Tanzania ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (Inter-Parliamentary Union – IPU) utakaofanyika jijini Arusha mwezi Oktoba 2026. Mheshimiwa Spika alieleza kuunga mkono mkutano huo na kusisitiza dhamira yake ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibunge kati ya Tanzania na Uingereza.

Mazungumzo hayo yalidhihirisha mwendelezo mzuri wa mahusiano kati ya Tanzania na Uingereza pamoja na dhamira ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa wananchi wa nchi zote mbili.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI