Header Ads Widget

TAWIRI WAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA


Chinangali Park, Dodoma


TAWIRI  imeendelea kutoa elimu  kwa wadau wakiwepo  wananchi ambapo wakulima wamepata elimu ya umuhimu wa wadudu katika  uhifadhi endelevu wa wanyamapori sambamba na mchango wa wadudu katika kilimo ikiwa ni pamoja na uchavushaji.

Vilevile wananchi wamepata uelewa  juu ya juhudi zinazofanywa na TAWIRI chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii za kuwahifadhi wanyamapori kwa kutumia taarifa sahihi za kisayansi.

“tunashukuru kwa elimu nzuri, kabla ya elimu hii nilijua wanyamapori wanakaa porini wanajihudumia lakini leo nimepata uelewa  wanyamapori wanatibiwa, wanahesabiwa, wanafuatiliwa mienendo yao kwa kutumia teknolojia” 

amesema  Enderesa Salla miongoni mwa wananchi waliotembelea banda la TAWIRI

TAWIRI tunawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kuja kupata elimu ya sayansi ya wanyamapori  kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza Utalii.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI