Header Ads Widget

WAKUFUNZI 25 VETA KWENDA FINLAND MAFUNZONI

 


Na Matukio DaimaApp 


Wazira wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema  ujuzi watakaoupata wakufunzi 25 wanaokwendwa nchini Finland utawezesha kuimarisha shughuli za madini na kuongeza ushindani wa madini ya Tanzania katika soko la kimataifa.


Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwaaga wakunzi hao kutoka Chuo cha Ufundi Stadi Veta, Prof Mkenda amesema kuwa Wizara ya elimu  inatarajia kuongeza idadi ya wataalamu wa kisasa katika sekta ya madini kupitia mafunzo yanayolenga kuinua ubora wa ufundi stadi nchini.


"Tunatarajia kupitia VETA, wataalamu wengi zaidi watazalishwa ili kusaidia kuongeza thamani ya madini yetu, nendeni mkafungue macho, mjifunze teknolojia mpya na mbinu bora zitakazokuwa na tija kwa Watanzania,"amesema  Prof. Mkenda.


Aidha, Prof Mkenda, amesema wakufunzi 25 wanaoelekea nchini Finland wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo ili kurejea na ujuzi utakaosaidia kukuza shughuli za uchimbaji na kuongeza thamani ya madini nchini.



Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema  mradi huo wa kimkakati unatarajia kuwafikia zaidi ya watanzania 400, hasa kutoka jamii zinazojihusisha na shughuli za uchimbaji madini, huku kipaumbele kikitolewa kwa wanawake na makundi maalum.


Ameongeza kuwa, wakufunzi hao watakaporejea wataeneza ujuzi kwa wenzao pamoja na kuwezesha kuanza kutumika kwa mitaala sita mipya, ikiwemo inayohusu sekta ya madini


Mwakilishi wa Wizara ya Madini, CPA Zephaniah Henry, amesema  bado kuna uhaba wa wataalamu wa uchimbaji madini nchini, hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuziba pengo hilo na kuongeza wataalamu wenye ujuzi wa kisasa.



Nae, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dk. Mwajuma Lingwanda, amesema  mradi huo utaongeza ubora wa mafunzo ya ufundi stadi katika sekta ya madini na kuleta matokeo chanya kwa taifa.


Mkufunzi kutoka VETA Dodoma, Neema Lyimo, amesema  wamebeba matumaini ya vijana wa Tanzania na wana dhamira ya kuimarisha sekta ya madini kupitia ujuzi watakaoupata.


Wakufunzi hao wanatarajiwa kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa kisasa wa madini (digital mining), usalama na afya migodini, utunzaji wa mazingira pamoja na uendeshaji wa mitambo ya kisasa inayotumika katika sekta hiyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI