Changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba watumishi wanaostaafu na wanaofariki wakiwa kazini zikiwemo za kushindwa kupata mafao yao kwa wakati na kutapeliwa zimeendelea kushughulikiwa na mfuko wa hifadhi ya Jamii PSSSF Ili kurahisisha utoaji huduma.
Miongoni mwa malalamiko ambayo yametajwa kufanyiwa kazi ni pamoja na gharama za ufuatiliaji ambazo zilikuwa zikifanyika kwa mfumo wa analojia na sasa kidigitali pamoja na kuwasaidia wasiojua namna ya kufuatilia mafao hayo kutokana na mlolongo wa ujazaji fomu ili kuziingiza kwenye mfumo.
Ofisa mfawidhi wa PSSSF Mkoa wa Njombe Andrew Dayson wakati wa mafunzo kwa wanahabari Mkoani Hapa juu ya huduma zinazotolewa na mfuko huo amesema hivi sasa watumishi na wastaafu wananufaika na mafao yao kwa wakati na yanashughulikiwa siku chache kabla mtumishi hajastaafu.
Baadhi ya wanahabari waliopatiwa mafunzo hayo akiwemo Jacob Mwenga na Ichikael Malisa wanasema matepeli wengi wanaowarubuni wastaafu kwa sasa wamedhibiti kwa kuweka mifumo ya kidigitali.
Hata hivyo jamii imeaswa kuwatumia wataalamu toka katika mifuko ya hifadhi ya jamii pindi wanapokwama badala ya kutafuta msaada kwa wasiowajua.














0 Comments