Header Ads Widget

WATENDAJI WATAKIWA KUTOKA OFISINI NA KUWAFUATA WANANCHI NA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

 


Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Erasto Sima, amewataka watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kubadili utendaji wao kwa kutoka ofisini na kuwafuata wananchi moja kwa moja ili kusikiliza na kutatua changamoto zao, ikiwemo migogoro ya ardhi ambayo imekuwa tatizo kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Bukoba.

DC. Sima ametoa melekezo hayo katiika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Bukoba cha kujadili taarifa za kamati mbalimbali, ambapo ameeleza kuwa miongoni mwa matatizo makubwa yanayowakabili wakazi wa wilaya hiyo ni migogoro ya ardhi, na kusisitiza umuhimu wa viongozi kuwa karibu na wananchi ili kupata ufumbuzi wa haraka na wa vitendo.

“watendaji tokeni ofisini wafuate wananchi wasikilizeni changamoto zao, migogoro ya ardhi imekuwa mingi kwa wananchi wetu, lakini unamkuta mtendaji anakaa ofisini wakati amepewa na gari kabisa lakini hawahudumii wananchi, juzi hapa katika nklini ya kusikilaza kero za wananchi tulipokea changamoto nyingi lakini mpaka sasa nyingine bado hazijatatuliwa”



Aidha katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ameitaka halmashauri kumaliza changamoto za wananchi mapema kabla hazijaenda nagzi nyingine ya juu wakati zinaweza kutatuliwa katika ngazi ya halmashauri.

“tujitahidi kutatua changamoto za wananchi mapema zisifike katika ngazi ya mkoa, mfano leo nimepigiwa na mkuu wa mkoa kuna mwananchi ameenda mpaka ofisi ya mkuu wa mkoa ili kupata ufumbuzi wa changamoto yake, tujitahidi kuwasaidia wananchi wetu”

Kwa upande wake mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba Acton Rwankomezi amesisitiza utekeelezaji wa maazimio ya baraza la madiwani ili kuhakikisha kila jambo linaloamuliwa na baraza hilo linafanyiwa kazi kwa manufaa mapana ya manispaa hiyo.



“nimegundua mambo mengi tunayoazima hapa hayafanyiwi utekelezaji jambao ambalo halina maana kwa baraza kuazimia jambo flani, nisisitize kila maazimio yanayoazimiwa hapa kuhakikisha yanafanyiwa utekelezaji na mimi nipate ripoti ya utekelezaji huo”

Naye katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bukoba mjini Shaban Mdoe amesisitiza wananchi kuepuka migogoro baina yao na wawekezaji katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ili kuchocheza maendeleo na ukuaji wa mji wa Bukoba na kukuza mapato ya halmashuri hiyo.

“nimesikia hapa kuhusu maeneo yalitengwa kwa ajili ya uwekezaji ni jambo zuri ila nisisitize sisi kama chama hatutaki kusikia migogoro baina ya wawekezaji na wananchi katika yale maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji njia sahihi za uwekezaji zifuatwe na wapatikane watu sahihi wa kuwekeza”

Katika barazo hilo taarifa za kamati mbalimbali ziliwasilisha huku msisitizo ukiwa katika miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika mji wa Bukoba kukamilika kwa wakati na ile ambayo bado haijaanza utekelezaji wake kuanza mara moja ili kutoa huduma kwa wananchi na kuwapunguzia adha ikiwemo mafuriko na ugumu wa kusafiri.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI