Header Ads Widget

MIILI MIWILI YAOPOLEWA DAR ES SALAAM

 


Na Matukio DaimaApp


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, limeopoa miili miwili iliyokua inaelea kwenye Maji  katika eneo la Stakishari Ukonga na Daraja la Sarenda na kuikabidhi kwenye vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kwa uchunguzi zaidi.


Kamanda wa jeshi hilo Mkoa wa Ilala ,SACF Mabusi Peter, akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Zimamoto Duniani, ambapo amefafanua kwamba katika eneo la Stakishari mwili wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 jana jioni  uliopolewa kwenye Maji.


Pia mwili mwingine wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 21 hadi 26 umeopolewa leo majira ya saa tano asubuhi katika daraja la Salenda.


"Leo asubuhi tukiwa katika viwanja hivi vya Mnazi Mmoja tulipokea taarifa ya wito kuwa kuna mwili wa mwanaume asiyefahamika umeonekana ukielea katika daraja la Salenda na tukaenda kuuopoa pia jana  tuliopoa mwili wa mwanamke maeneo ya Stakishari, miili hiyo tumeikabidhi kwenye vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya ichunguzi"amesema SACF Mabusi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI