Na John I Bera, Ndutu - Arusha
Timu ya Safari Field Challenge imepongezwa kwa mchango wake katika kuongeza ujuzi na ufanisi wa waongoza utalii ambayo ni chachu ya kutangaza utalii na kuimarisha uhifadhi nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kutembelea timu hiyo katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Ndutu, ambapo ameisifu kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania ndani na nje ya mipaka yake.
“Niwapongeze kwa kazi hii njema. Nimeambiwa hii ni Safari Field Challenge ya kumi na moja, hongereni sana kwa kuutangaza utalii,” amesema Dkt. Kijaji.
Ameongeza kuwa kazi wanazofanya inaunga mkono juhudi za serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye aliutangaza utalii wa Tanzania kupitia filamu maarufu ya Tanania: The Royal Tour, iliyotumika kuitangaza nchi kimataifa kama kitovu cha vivutio vya utalii.
Sambamba na hayo, Dkt. Kijaji alisisitiza umuhimu wa kuendelea kubuni na kuwasilisha vivutio vipya ili kuongeza idadi ya watalii na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.]
Vilevile, aliitaka timu hiyo kutumia jukwaa lao kutangaza vivutio mbalimbali, ikiwemo uwanja mpya wa gofu katika eneo la Serengeti pamoja na hazina nyingine za kipekee za nchi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, amesema jitihada za Safari Field Challenge zina mchango mkubwa katika kuongeza uelewa wa umuhimu wa uhifadhi wa maliasili, hasa kwa vijana na jamii kwa ujumla.]
Naye mwanzilishi wa Safari Field Challenge, Bw. Sadock Mgeta ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutambua mchango wa waongoza Utalii na kuiwezesha Safari Field Challenge kuendelea kufanyika kwa miaka 11












0 Comments