Header Ads Widget

MAMIA WAJITOKEZA KAMBI YA MADAKTARI MABINGWA WA MACHO KIGOMA

 

Mlezi wa taasisi ya Lalji Foundation Mohsin Abdallah Sheni akizungumza wakati wa uzinduzi wa kambi ya siku nne ya madaktari bingwa wa macho mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Zaidi ya watu 1500 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa Kigoma wamejitokeza katika siku ya kwanza kati ya siku nne za kambi ya matibabu ya Kibingwa ya Macho inayofanyika mjini Kigoma kwa uratibu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Lalji Foundation.

Mlezi wa Taasisi ya Lalji Foundation, Mohsin Abdallah alisema kuwa hadi kufikia mchana April 3 siku ya kwanza ya kambi hiyo  idadi kubwa ya watu walikuwa wamejitokeza kupata huduma hiyo ambayo itadumu kwa siku nne . 

Abdallah alisema kuwa katika kambi hiyo jumla ya madaktari bingwa, wahudumu wa afya na wataalam mbalimbali 28 kutoka jijini Dar es Salaam watatoa huduma kwenye kambi hiyo huku madaktari bingwa na wahudumu na wataalam 10 kutoka Hospitaali ya mkoa Kigoma maweni watasaidia katika utoaji huduma ambapo watu 6000 wanatarajia kufikiwa na operesheni Zaidi ya 500 za macho zitafanyika.

Akizindua kambi hiyo ya matibabu Mkuu wa mkoa Kigoma, Balozi Simon sirro alisema kuwa kambi hizo za matibabu ya Kibingwa zimekuwa na msaada mkubwa kwa wananchi wa kawaida kusogeza huduma lakini pia kusaidia wananchi wasio na uwezo kupata huduma hizo kwa karibu.

Balozi Sirro alisema kuwa binafsi amechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kufanyika kwa kambi hiyo ambayo imepata Baraka za wizara ya afya ambayo inatambua mchango wa sekta binafsi katika kusaidia huduma za afya na huduma mbalimbali za kijamii nchini.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI