Header Ads Widget

CBE YAENDELEA KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA KUPITIA SERA NA MAFUNZO

 

NA MWANDISHI WETU , DAR ES SALAAM

Imeelezwa kuwa usawa wa kijinsia unaendelea kuwa nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuimarisha utawala bora katika jamii na taifa kwa ujumla.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Jinsia Duniani yaliyofanyika katika College of Business Education (CBE), Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, amesema kuwa usawa wa kijinsia ni msingi wa maendeleo jumuishi.

Amesema juhudi za taasisi mbalimbali, ikiwemo CBE, katika kuimarisha usawa wa kijinsia kupitia sera, mifumo na programu, zimekuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taasisi na taifa kwa ujumla.

“Ni muhimu kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia unapewa kipaumbele katika sekta zote ili kufikia maendeleo endelevu na jumuishi,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkuu wa CBE, Profesa Edda Lwoga, amesema chuo hicho kimeendelea kutekeleza mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia fursa za uongozi na maendeleo ya kitaaluma.

Amefafanua kuwa kila mwaka watumishi hupatiwa mafunzo kuhusu usawa wa kijinsia, huku wanafunzi wakielimishwa juu ya umuhimu wa kuheshimiana na kushirikiana bila ubaguzi.

Aidha, hatua mbalimbali zikiwemo kuanzishwa kwa dawati la jinsia, utoaji wa mafunzo endelevu, pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi, zimetajwa kuwa chachu ya maendeleo ndani ya chuo hicho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI