Header Ads Widget

MWINGIZAJI MKONGWE HASHIM KAMBI AFARIKI DUNIA

Tasnia ya filamu nchini imepata pigo kubwa kufuatia taarifa za kifo cha msanii mkongwe Hashim Kambi, aliyefariki dunia akiwa hospitalini baada ya kuzidiwa ghafla wakati akifanya shughuli zake za kurekodi studio.

Marehemu Hashim Kambi alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliolitumikia kwa muda mrefu tasnia ya Bongo Movie, akijizolea heshima kubwa kutokana na umahiri wake wa uigizaji hasa kwenye majukumu ya uhusika wa watu wazima yenye mafundisho ya kijamii.

Kupitia kazi zake, ameacha alama ya kudumu kwenye mioyo ya watazamaji wengi, huku akichukuliwa kama mmoja wa waasisi na walezi wa vipaji vipya ndani ya tasnia ya filamu Tanzania.

Kifo chake ni pigo si tu kwa familia na ndugu, bali pia kwa wadau wote wa sanaa na burudani nchini.


Taarifa zaidi kuhusu msiba na taratibu za mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia pamoja na wahusika wa karibu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

USISAHAU KUTEMBELEA  CHANEL YA Matukio Daima online  NA KU subscribe 

#MatukioDaimaTIKTOK

#MatukioDaimaTv

#www.matukiodaimahabari.co.tz



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI