NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Na Hadija Omary
LINDI....Kupeleka kilele cha siku ya wanawake Duniani mayo uadhimishwa March 8 kila mwaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua kliniki maalum iitwayo Samia Ardhi Kliniki Mkoa wa Lindi yenye lengo la kuongeza idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi,
Uzinduzi huo umefanyika huko manispaa ya Lindi Mkoani Lindi na Mkuu wa Wilaya hiyo Victoria Mwanziva ambapo amewataka Wanawake wa Mkoa huo kujitokeza kwa wangi kutumia fursa ya kliniki hiyo kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali, .
Mwanziva Amesema hatua hiyo inalenga kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha huduma za ardhi zinatolewa kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya usawa wa kijinsia.
Mwakilishi wa kamishina wa Aridhi Mkoa wa Lindi Bi. Rabeca Mjanja amesema lengo kuu la Samia Ardhi Kliniki ni kuongeza asilimia ya umiliki wa ardhi kwa wanawake nchini kupitia utoaji wa elimu, hati za umiliki na utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Amesema kampeni hiyo inaendeshwa Nchi mzima ambayo imeanza rasmi march 2 na inatarajiwa kutamatika machi 7 mwaka huu ambapo wanawake Katika Mikoa husika watanufaika na kampeni hiyo
Amesema mpango huo unalenga kuhakikisha changamoto zinazowakabili wanawake katika sekta ya ardhi zinatatuliwa kwa wakati, huku ukichochea ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla.
Amefafanua kuwa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 iliweka msingi wa usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi kati ya wanaume na wanawake. Hata hivyo, amesema changamoto zilijitokeza katika utekelezaji, hasa kwenye masuala ya mirathi na urithi ambapo mila na desturi zilichangia kuwabagua wanawake.
Aidha amesisitiza kuwa katika sera hiyo mpya, masuala ya urithi na mirathi yameainishwa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, hivyo kuweka mazingira rafiki kwa wanawake kumiliki na kurithi ardhi bila ubaguzi.
Bi.bibie Mwambe mkazi wa Lindi mjini ni miongoni mwa Wanawake walioanza kunufaika na klinik hiyo kwa kupata hati amemshukuru Rais kwa kuwapa kipaumbele wanawake na kuwasihi wale ambao bado hawajajitokeza kufanya hivyo ili kunufaika na huduma hiyo.
MWISHO.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)






0 Comments