Na Francis Godwin ,Matukio Daima Media
Tanzania ni mkakati kabambe wa kuepukana na Matumizi ya nishati ya kuni na mkaa, maarufu kama nishati chafu ya kupikia na kuelekea kwenye mapinduzi ya Nishati safi yenye kutunza mazingira .
Ni jitihada kubwa zimeendelea kufanywa na Serikali , wadau mbalimbali nchini na duniani kuhimiza matumizi ya nishati safi kwa lengo la kuboresha afya, kulinda mazingira, na kupunguza athari za mabadiliko ya tabiaNchi.
Angelina Kadinde, mjasiriamali wa kuni kutoka Iringa, anasema biashara ya kuni kwa sasa wateja wamekuwa wachache kutokana na wengi wao kuelekeza nguvu katika matumizi ya Gesi .
Alisema miaka ya nyuma alikuwa akiuza kuni kwa siku zaidi ya mizigo 20 hadi 45 ila sasa hata mzigo mmoja kwa siku ni shida .
"Kila mteja ninayempelekea kuni anasema anatumia Gesi ama ana jiko la umeme la kupikia hivyo najikuta nabaki na kuni bila wateja "
Hata hivyo alisema kutokana na upatikanaji wa kuni kuwa mgumu gharama ya mzigo wa kuni amekuwa juu .
"Watumiaji wengine wa kuni wanaona changamoto ya gharama kama kikwazo kikuu kwao ndio maana wamehamia kwemye ges"
Bitrisi Shabani, mmoja wa wakazi wa Miyomboni katikati ya mji wa Iringa, anasema pamoja na gharama kubwa za kujaza mitungi ya gesi bado gesi inamsaidia zaidi kuliko kuni.
Kuwa matumizi ya gesi kwa sasa yamekuwa ni habari ya mjini hivyo kuathiri biashara ya kuni kama .
Kwani alisema mzigo wa kuni wa kutumia wiki moja unauzwa Tsh 30,000 ama 25,000 wakati mtungi wa Gesi mdogo ni kati ya Tsh 24,000 na unaweza kutumia mwezi mzima ama wiki tatu.
Hivyo alisema ukilinganisha na gharama ya kuni ama mkaa unaouzwa gunia kati ya Tsh 25,000 hadi 32000 bado matumizi ya gesi ni nafuu zaidi.
Bado alisema changamoto ya kuni na mkaa upatikanaji wake kwani wafanyabiashara wamekuwa wakiogopa kuuza mchana kutokana na kutokuwa na vibali vya kufanyabiashara hiyo.
Mfanyabiashara wa majiko ya gesi mjini Iringa, kwamba awali wateja wengi waliokuwa wananunua majiko hayo ni wanafunzi wa vyuo Zaidi ila kwa sasa idadi kubwa ya wananchi wananunua majiko hayo kutokana na elimu kubwa ambayo imekuwa ikitolewa.
Serikali kupitia mikusanyiko mbali mbali zikiwemo nyumba za ibada imeluwa ikitoa elimu ya matumizi ya nishati safi .
Huku viongozi wa dini pia wameishukuru serikali kwa elimu inayotolewa na kushauri serikali kuhakikisha bei za gesi inaendelea kushuka ili kila mwananchi aweze kutumia Gesi kupikia.
Wameongeza kuwa matumizi ya kuni na ukataji miti kiholela vinakiuka maadili ya kidini na kuhatarisha mazingira, hali inayohitaji hatua madhubuti za upandaji miti ili kurejesha uoto wa asili.
Mchungaji wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Afrika mashariki (KKKAM) Titus Kiungo mbali ya kupongeza serikali kwa mkakati wa kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya Kupikia Bado anashauri bei ya Nishati hiyo iwe rafiki kwa Kila mmoja ili matumizi yaongezeke zaidi .
Kuwa changamoto kubwa ni gharama ya ujazaji gesi baada ya Kuishi mtanzania wa kipato Cha chini hawezi kumudu bei hiyo .
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwanda, amesema kuwa matumizi ya nishati safi ni njia mojawapo ya kukabiliana na ongezeko la joto katika mkoa huo.
Kuwa matumizi ya nishati safi si tu yanaboresha afya bali pia huokoa muda wa kupika na kuboresha hali ya maisha.
Alisema ni kuwa Nishati Safi ya Kupikia na agenda ya matumizi ya nishati safi imepewa kipaumbele katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa .
Lengo likiwa ni Kulinda Mazingira na
Manispaa ya Iringa imeanzisha kampeni ya kupanda miti ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mwongozo wa Benki ya Dunia wa mwaka 2020 unasisitiza kuwa nishati safi hupimwa kwa vigezo kama ufanisi, usalama, urahisi wa matumizi, unafuu wa gharama, na kiwango kidogo cha sumu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linapima teknolojia safi kulingana na kiwango cha hewa hatarishi kama kaboni monoksidi na chembechembe za vumbi zinazotolewa wakati wa kupikia.
Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi 2024-2034
Tanzania imeanzisha Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034, ukilenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipouzindua mkakati huu, alieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mkakati huu pia umepokewa vyema na taasisi mbalimbali kama Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira, pamoja na wanasiasa.
Wadau hawa wamejitolea kutoa elimu na kusaidia kaya zenye uhitaji kupata majiko ya nishati safi.
Aina za Nishati Zinazotumika Nchini
Nchini Tanzania, aina za nishati za kupikia ni pamoja na kuni, mkaa, mafuta ya taa, bayogesi, bayoethanol, gesi asilia, LPG, umeme, majiko banifu, na majiko yanayotumia nishati ya jua.
Hata hivyo, kulingana na ripoti ya Cooking Energy Action Plan ya mwaka 2022, asilimia 90 ya kaya nchini bado zinategemea kuni na mkaa, ambapo kuni hutumika kwa asilimia 63.5 na mkaa kwa asilimia 26.2.
Athari za Kiafya na Mazingira
Matumizi ya nishati chafu yameleta changamoto nyingi kiafya.
Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya 30,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa yanayohusiana na matumizi ya nishati chafu, huku wanawake na watoto wakiwa waathirika wakuu.
Ni ukweli kuwa kwa kutumia nishati safi, mtu anaweza kupunguza muda wa kupika kutoka saa saba kwa wiki hadi saa moja.
Mkakati huu wa nishati safi, elimu na upatikanaji wa nishati ya gharama nafuu vinapaswa kupewa kipaumbele.
Hivyo Serikali, wadau wa maendeleo, na wananchi wanapaswa kushirikiana kuhakikisha mabadiliko ya kudumu na endelevu yanafikiwa.





0 Comments