Tarehe 03 Machi, 2026 kila mwaka ni maadhimisho ya Siku ya Wanyamaporo Duniani. Kwa mwaka huu maadhimisho haya kitaifa yafanyika ndani ya Jiji la Arusha viwanja vya (NANE)88- Njiro.
"TAWIRI tupo na tunajivunia mchango mkubwa katika uhifadhi wa rasilimali ya Wanyamapori kupitia taarifa za kisayansi ambapo takwimu na taarifa za tafiti hutumika kuhifadhi wanyamapori sambamba na kunadi utalii."
Aidha, majukumu ya TAWIRI yamejikita katika ustawi wa uhifadhi wa Wanyamapori na kukuza utalii nchini ikiwa ni pamoja na kufanya, kuratibu na kusimamia tafiti za wanyamapori. Kufanya sensa ya wanyamapori, kufanya matibabu kwa wanyamapori nk
Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni "MIMEA DAWA, NA MANUKATO: KUTUNZA AFYA, KUHIFADHI URITHI NA KUBORESHA MAISHA"

.jpg)








0 Comments