Header Ads Widget

TFS TABORA YAPANDA MITI 1,000 KUADHIMISHA SIKU YA MISITU DUNIANI

 


Wananchi wahimizwa kuitunza ili iwe chachu ya uchumi endelevu


TABORA, Machi 19, 2026 — Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda na Wilaya ya Tabora kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama, watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora pamoja na wananchi, leo imeadhimisha kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Kampeni ya Upandaji Miti Kitaifa kwa kupanda miti 1,000.

Zoezi hilo limefanyika katika Shule ya Sekondari Fundikira iliyopo Kata ya Kiloleni, Manispaa ya Tabora, ambapo miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda, mbao, kivuli pamoja na ya kuhifadhi vyanzo vya maji imepandwa.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora, Bi. Asha Churu, ambaye aliwataka wananchi na wadau wote kuhakikisha miti iliyopandwa inalindwa na kutunzwa ili iwe na tija kwa jamii.

Alisema uhifadhi wa misitu ni jukumu la kila mwananchi kwa kuwa una mchango mkubwa katika ustawi wa uchumi na maisha ya kizazi cha sasa na kijacho, huku akisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Zoezi hilo ni sehemu ya utekelezaji wa kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Misitu ni Uchumi Endelevu, Tuhifadhi kwa Maendeleo ya Kitaifa.”

Wananchi wa eneo hilo walishiriki kikamilifu katika upandaji miti na kuahidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha miti iliyopandwa inalindwa na kukua kwa manufaa ya jamii.














Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI