TUKIO la kikatili limetokea katika Kijiji cha Changarawe wilayani Kilosa mkoani Morogoro baada ya kugundulika mwili wa mwanamke mmoja ukiwa umefukiwa ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi na rafiki yake wa kiume Khalid Mavuze ambaye naye ametoweka.
Mwanamke huyo ametambuliwa kwa jina la Lilian Danstan Manga (27) ambaye aliripotiwa kutoweka tangu Desemba 11, 2025 katika Kitongoji cha Kipera, Kata ya Masanze.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, mwili huo uligunduliwa baada ya mwanamke aliyekuwa akifanya usafi katika nyumba hiyo kubaini tuta la udongo ndani ya chumba.
“Baada ya taarifa hiyo kupokelewa, uchunguzi ulifanyika na hatimaye mwili wa mwanamke huyo kufukuliwa ndani ya nyumba hiyo,” alisema.
Baba wa marehemu, Danstan Albano Manga, amesema familia imepata pigo kubwa kufuatia tukio hilo.
Naye Felista Simon, jirani na mkazi wa Changarawe, amesema tukio hilo limewatia hofu wakazi wa eneo hilo.
“Hatukutarajia kabisa tukio la aina hii kutokea katika kijiji chetu,” alisema.
Kwa upande wake Nicholous Mkoma,Mwenyekiti wa Kijiji cha Changarawe, amesema viongozi wa kijiji walichukua hatua za haraka baada ya kupokea taarifa.
Nyumba mwili ulipo kutwaMkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu tukio hilo huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi.
Akatoa pole kwa waliofikwa na msib
a huo na kuonya tabia ya watu kujichukulia Sheria mkononi, badala yake watumie Vyombo vya Dola, mamlaka mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, dini na watu wengine kusuluhisha matatizo yanayoibuka kwenye jamii
.

.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)

.jpg)




0 Comments