Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), leo imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 103 kutoka kwa Uongozi wa King James Pharmacy ya jijini Mbeya katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika maboresho ya huduma ya afya nchini .
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa King James Pharmacy, Dkt. Gloria Mbwile ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Saia Suluh Hassan Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapinduzi makubwa katika sekta ya afya .
"Tumeamua kutoa msaada huu ili kuunga mkono juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi. Tunaona uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye miundombinu na vifaa tiba nchi nzima, hivyo kama wadau wazawa, tumeona ni wajibu wetu kuungana na Serikali katika kuhakikisha huduma bora zinafika kwa kila mwananchi."
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameeleza kufarijika sana na hatua hiyo ya kizalendo.
"Ni mabadiliko makubwa ya kifikra kuona wadau wazawa kama King James wakiona haja ya kutoa sadaka na michango yao kwa taasisi za afya nchini. Msaada huu utaacha kumbukumbu nzuri kwa hospitali na wagonjwa watakaohudumiwa," alieleza Dkt. Mbwanji
Nao watumiaji wa vifaa hivyo, Muuguzi Mkuu wa Hospitali, Petro Semen, pamoja na Seraphine Mushi Mkuu wa Kitengo cha fiziotherapia, wamesema kuwa vifaa hivyo vya kisasa vitaongeza ufanisi na kupanua wigo wa utoaji huduma kwa wagonjwa, huku wakiahidi kuvitunza ili vidumu kwa muda mrefu.
Msaada huo uliotolewa maalum katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, unajumuisha vifaa muhimu kwa ajili ya Idara ya Tiba kwa Vitendo (Physiotherapy), Wodi ya Watoto, pamoja na Kitengo cha Uangalizi Maalum (ICU).









0 Comments