![]() |
| Dkt. Angela Mwakatobe |
Wanawake wameendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sayansi, utafiti na uongozi, kupitia taaluma, juhudi na uthubutu.
Miongoni mwa wanawake wanaoonesha mafanikio hayo ni Dkt. Angela Mwakatobe, ambaye ni mwanasayansi na kiongozi anayeshiriki kikamilifu katika uhifadhi wa rasilimali ya wanyamapori kupitia Utafiti.
Dkt.Mwakatobe ni Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Magharibi kilichopo Kigoma, ambacho ni miongoni mwa Vituo vitano vya utafiti vilivyo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Uongozi wake katika Kituo hicho ni nguvu ya gurudumu la kufanya, kuratibu na kusimamia tafiti za wanyamapori wanaopatikana katika ukanda wa magharibi na kuhimiza matumizi ya taarifa za kisayansi katika uhifadhi wa wanyamapori, hususani spishi adimu kama Sokwe.
Dkt.Mwakatobe ni taswira ya uimara wa mwanamke katika Uongozi maendeleo ya Kisayansi






0 Comments