Header Ads Widget

MIKOPO YA HALMASHAURI YACHOCHEA AJIRA KWA VIJANA

Mwenyekiti wa kikundi cha vijana wa bodaboda kijiji cha Makere, George Kagoma


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MILIONI 70 zilizotolewa kwa madereva pikipiki katika kijiji cha Makere wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imewezesha vijana Zaidi ya 20 wa kijiji hicho kununua pikipiki na kujiajiri hali iliyowafanya kuendesha maisha yao kwa ufanisi.

Vijana hao ambao awali walikuwa wakiendesha gari ndogo za kubeba abiria kutoka Makere kwenda Kasulu mjini na Kibondo maarufu kama mchomoko wakizungumza na waandishi wa habari walisema kuwa mikopo inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani imetengeneza ajira kubwa kwa vijana mbalimbali.

Mwenyekiti wa kikundi cha vijana wa bodaboda kijiji cha Makere, George Kagoma alisema idadi kubwa ya vijana waliopata pikipiki walikuwa madereva wa gari ndogo lakini waliona maslahi wanayopata hayakidhi kuendesha maisha yao ndipo wakaanzisha kikundi hicho na kuomba mkopo kununua pikipiki.

Kwa upande wake Katibu wa kikundi hicho, Julius Stephen ameisshukuru serikali ya Rais Samia kwamba kuwezesha kupata mkopo huo ambao umewezesha vijana kujiajiri na kwamba tangu wamepata mkopo huo mwezi januari mwka huu tayari wamesharudisha milioni 10.

Afisa Mtendaji wa kata ya Makere, Sixmund Katto akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 134.5 zimetolewa kwa vikundi vitano vya vijana na wanawake ambaao wanaendesha shughuli zao za kiuchumi na kwamba vikundi vingine 14 vipo kwenye mchakato.

Makere, Sixmund Katto 


Baadhi ya pikipiki zinazomilikiwa na wanachama wa kikundi cha bodaboda Makere wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI