Header Ads Widget

MARIAM CHUMA KOBELO, CHUMA CHA MJERUMANI NGORONGORO



“Kwa Mungu hakuna kubwa kwa kuwa hashindwi kitu, tusikate tamaa katika kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio vya utalii, ipo siku watanzania wanaotembelea vivutio vya utalii Ngorongoro na maeneo mengine watakuwa wengi zaidi”.

Maneno kutoka kwa Mariam Chuma Kobelo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za utalii na Masoko Ngorongoro akielezea umuhimu wa utalii wa ndani kwa watanzania.

Ni jembe la Ngorongoro na katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Ngorongoro tunatambua mchango wake  kwa kubuni kampeni mbili za kuhamasisha utalii wa ndani na kuibua mazao mapya ya utalii kama *Wedding Tourism* 

Ubunifu wa kampeni za _Merry and Wild Ngorongoro Awaits_ na _Diko la Amboni_  ni mawazo yake yaliyosaidia kuongeza idadi ya watalii wa ndani na kuibua vivutio vipya vya utalii.

Chukua maua yako mama kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2026.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI