Header Ads Widget

UPENDO PORINI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA MIKUMI


Mshindi wa awamu ya tatu wa kampeni ya Upendo Porini, Yona Samwel (@snipertaget) na mpendwa wake Foibe wameendelea na safari yao ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi. Washindi hao walipokelewa kwa shangwe na uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, kisha walipongezwa kwa ushindi wao kwa kuichagua Hifadhi hiyo ya kipekee katika Kampeni ya #UpendoPorini. Pongezi hizi ziliambatana na kupewa zawadi kama kumbukumbu ya kuitembelea Hifadhi hiyo.

Baada ya mapokezi hayo, Yona na Foibe walifurahia utalii wa kuangalia wanyama(game drive), ambapo walibahatika kuona wanyamapori mbalimbali ndani ya muda mfupi wakiwemo Tembo, Simba, Twiga, Viboko,Pundamilia na mandhari ya kipekee ya Hifadhi ya Taifa Mikumi.

Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @tanzaniaparks kwa taarifa zaidi za  Hifadhi za taifa Tanzania. 

#UpendoPorini #TanzaniaParks #Mikumi #DestinationTanzania












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI