NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeyatupilia mbali mapingamizi yaliyowasilishwa na Said Issa Mohammed na wenzake kupinga kuunganishwa kwa Tundu Lissu katika kesi ya mgawanyo wa mali inayomkabili Katibu Mkuu wa CHADEMA pamoja na Bodi ya Wadhamini.
Uamuzi huo umetolewa leo Machi 03, 2026 na Jaji Hamidu Mwanga, ambaye aliyatupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na Wakili wa walalamikaji, akieleza kuwa hayakuwa na msingi wa kisheria wa kuzuia maombi ya kuunganishwa kwa Lissu katika shauri hilo.
Kwa mujibu wa ratiba ya mahakama, kufuatia uamuzi huo, maombi ya msingi yaliyowasilishwa na Lissu yatasikilizwa Ijumaa, Machi 06, 2026, saa tatu asubuhi mbele ya Jaji Hamidu Mwanga.
Kesi hiyo ya mgawanyo wa mali imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu kutokana na uzito wake kisiasa na kisheria ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
MWISHO.





0 Comments