![]() |
| Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa na waombolezaji wengine katika tukio hilo |
Na. Sixmund Begashe, Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 27 Machi 2025 ameungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), Wabunge na viongozi wengine katika ibada ya kuaga miwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Ismani Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Mhe. Lukuvi aliyefariki tarehe 25 Machi 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Paulo wa Msalama Jimbo Kuu Dodoma Padri Simon Mswaga katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
![]() |
| Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwasili katika tukio hilo |










0 Comments