Na. Mwandishi Wetu, Dar.
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Jenga Hub wameandaa App maalum "KALIMANI APP" kwa ajili ya kusaidia Wanafunzi viziwi wa Darasa la Awali, la Kwanza na la Pili, kwa kutumia Mtaala ulioboreshwa wa Mwaka 2023 na Kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania.
Akifunga rasmi kikao kazi cha siku tatu Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba leo tarehe 27/3/2026 cha kuandaa maudhui ya Kuhesabu katika hiyo ya “Kalimani App”
Amesema, maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 yemejikita katika kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa ni jumuishi na kuwa hakuna mtoto hata mmoja anayeachwa.
"Wazazi wenye watoto wenye mahitaji maaalum naomba muwapeleka shuleni kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeandaa mazingira wezeshi kwa watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu."amesema Dkt.Komba
![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba |
Pia , amewashukuru Jenga Hub kwa maono na ubunifu wao katika kuandaa App hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kisayansi wa KKK, uliozinduliwa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Vilevile, ameeleza kuwa TET itashirikiana kwa ukaribu na Jenga Hub kuhakikisha kuwa lengo la kuandaa App linafikiwa na kuwa App hii inawanufaisha walengwa wote nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jenga Hub iliyobuni Kalimani App, Bi Nancy Sumari, ameeleza kuwa App hii imelenga kutumiwa na watoto viziwi wa Darasa la Awali, Darasa la Kwanza, Pili na la Tatu.
![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Jenga Hub iliyobuni Kalimani App, Bi Nancy Sumari |
Aidha, ameeleza kuwa Kalimani App inaandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jenga Hub na TET na kuwa itawawawezesha watoto viziwi kujifunza Kuhesabu kwa urahisi na hivyo kuhakikisha lengo la serikali la kuwawezesha wanafunzi kuweza kuhesabu kwa ufasaha kabla ya kufika Darasa la Tatu linafikiwa.
Hata hivyo ,Bi Nancy ameishukuru sana TET kwa kuwa tayari kushirikiana na taasisi ya Jenga Hub katika kuhakikisha kuwa watoto viziwi nao wanapata haki yao ya msingi ya kupata vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

















0 Comments