Header Ads Widget

WANANCHI DAR ES SALAAM WAPONGEZA POLISI, UDHIBITI WA UHALIFU NA WAHALIFU


Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamepongeza na kuishukuru serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kudumisha amani na usalama nchini, suala linalowezesha wananchi hao kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Wananchi hao akiwemo Mjasiriamali Bi. Julieth Masaki, Mkazi wa Ilala, Jijini Dar Es Salaam ameeleza kuwa kuimarika kwa amani na usalama kunatoa ari na morali kwa wananchi kujikita katika biashara na shughuli nyingine za kiuchumi, akiipongeza serikali pia kwa udhibiti mkubwa wa uhalifu na wahalifu.

Bi. Masaki amemuomba Mwenyenzi Mungu kuendelea kuilinda Tanzania na kudumisha amani iliyopo nchini, akisisitiza pia ushiriki wa kila Mtanzania katika kulinda amani, umoja na mshikamano uliopo nchini.

"Nafarijika sana kuona Vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kuwajibika na kutuhakikishia ulinzi na usalama suala linalotupa nafasi ya kufanya kazi zetu jwa uhuru na amani. Niwaombee weledi zaidi katika kutimiza wajibu wao." Amesema Bi. Julieth Masaki.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI