Header Ads Widget

MWENYEKITI BARAZA LA VYAMA VYA SIASA: MIGOGORO IPUNGUE, WANAWAKE, VIJANA,WALEMAVU WAPATE NAFASI.

 


Na Matukio Daima, Morogoro

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Bw. Juma Ali Khatibu, amezihimiza chama cha siasa nchini kuimarisha mshikamano na kupunguza migogoro ya ndani ili kuimarisha demokrasia na ushirikishwaji wa makundi yote, hususan wanawake, watu wenye ulemavu na vijana.

Akizungumza mjini Morogoro wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya siasa, Bw. Khatibu alisema baraza lake linalenga kuona migogoro inapungua au kumalizika kabisa, huku nafasi za uongozi zikigawanywa kwa haki.


Alisema vyama vina wajibu wa kuhoji, kushauri na kushiriki kikamilifu katika kujenga Taifa kupitia ushauri kwa Serikali.

Kwa upande wake, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza, aliwahimiza viongozi kuhakikisha wanazingatia masuala ya kijinsia ili kuwapa wanawake nafasi ya kushiriki siasa.


Alisema demokrasia ya kweli lazima iwe shirikishi kwa kuhakikisha wanawake na wanaume wanashiriki kwa uwiano sawa.

Mafunzo hayo yalihusisha majadiliano kuhusu marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, gharama za uchaguzi, sera za jinsia na kanuni za mwaka 2025.


Katibu wa United Demovratic Party UDP, Bi. Swaum Rashid, amesema mafunzo hayo yataisaidia nchi kudumisha amani na utulivu.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI