Header Ads Widget

USHIRIKIANO WA JICA NA SUA YAIFANYA SERIKALI KUTENGENEZA VITUO 1,000 VYA KUHIFADHI MASHINE ZA KILIMO

 

Na Lilian Kasenene, Morogoro

Matukio DaimaApp 


WAKATI Tanzania ikifanya juhudi za uendelezaji wa kilimo ambacho kitahitaji matumizi ya mashine za kisasa, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa makusudi imeamua kutengeneza vituo zaidi ya 1,000 vya kuhifadhi mashine ambazo zitapatikana kwa urahisi ili wananchi waboreshe kilimo chao.


Naibu katibu mkuu(Maendeleo ya mazao na usalama wa chakula kutoka Wizara ya Kilimo Profesa Peter Msoffe alisema hayo mjini Morogoro alipomwakilisha Katibu mkuu Wizara hiyo wakati wa jukwaa la kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Japan kupitia Shirika la ushirikiano wa kimataifa la Japan(JICA) na Chuo kikuu Cha Sokoine Cha kilimo SUA .


Alisema yote hayawezi kufanikiwa bila kutilia mkazi uendelezaji wa kilimo, na kilimo sio kile kinachofahamika cha kutumia mkono bali ni kilimo kitakachotumika kwa mashine ndo maana Serikali baada ya kufanya uamuzi wa kutengeneza vituo ambavyo vitahifadhi,vinafanyia matengenezo, na kuzifanya mashine kupatikana kwa uraisi.


Prof Msoffe alisema Serikali inapozungumzia suala la kilimo kuboreshwa si kwa maneno tu bali ni kwa vitendo,kwamba tayari vituo vimeanzishwa na Serikali inatoa ruzuku ya mbolea,na pembejeo mbalimbali.


Akizungumzia uzoefu wa Serikali Japani katika kubadilisha kilimo kutumia mashine itakuwa ni muhimu na ni kama darasa kwa ajili ya Tanzania kujifunza namna Bora ya kutumia mashine.

Jukwaa hilo limekuwepo takribani miaka minne na ni jukwaa ambalo wataalamu wake ukutana na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusiana na kubadilishana uzoefu wa masuala ya Kilimo hasa katika matumizi ya mashine za kilimo kati ya Japan na Tanzania.

"Kama mnavyonfahamu Tanzania inapitia mabadiliko makubwa ya kilimo,lakini baada ya kipitishwa kwa dira ya 2050 Tanzania iko tayari kwa ajili ya kuongeza kwa Kasi Maendeleo yake ya kiuchumi ili kufikia nchi yenye uchumi wa takribani Dola tirioni 1 ifikapo 2050 na kipato cha mwananchi wa kawaida afikie Dola 7,000 lakini iwe nchi ya kipato cha kati," alisema.


Mwakilishi mkuu wa JICA Tanzania Ara Hitoshi akizungumza wakati wa jukwaa hilo alisema walianza ushirikiano kati ya JICA na SUA ulianza 2022, na Japani inatoa uzoefu wake kwenye shughuli za Maendeleo hasa Vijana

Kilimo ni Moja ya sekta muhimu na itasaidia na kuwafundisha Vijana namna Japani inavyolima kwa kutumia mashine na kwamba kupitia jukwaa hilo ni imani yake ni kuhakikisha Vijana wanawezeshwa kwenye kilimo hasa cha kisasa Cha kutumia teknolojia kama mashine na kuachana na kilimo Cha maziea.


"Nafikiri kilimo ni sekta muhimu kwa Tanzania tunapenda katika programu hii kushirikiana kwenye suala la kilimo,Japan na Tanzania wataalamu wake leo watatoa uzoefu wao kwenye mambo mbalimbali na vitu muhimu na hasa tumelenga Vijana wa Tanzania,"alisema
 
Afisa mwandamini katika sayansi, teknolojia na ubunifu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Edwin Konzo, alisema ili kufika dira ya 2050 ipo haja ya kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali ya kisera na Wizara inachukua nafasi ya kufanya mapitio upya wa sera ya sayansi na teknolojia ya Mwaka 1996 ili kuendana na mipango ya kiutekelezaji iliyopo katika dira.

Konzo alisema masuala ya Kilimo ndio injini ambayo unaweza kutoa mabadiliko,ili kuwe na mabadiliko katika kilimo tunahitaji Teknolojia na bunifu mbalimbali.

"Mkutano huu unajaribu kubadilishana uzoefu wa kujifunza kutoka teknolojia ambao Japan wametumia katika mabadiliko ili wataalamu wajifunze kutoka katika Maendeleo ya Kilimo na kufikia hatua mbalimbali na kuwafanya watanzania kuweza kutumia teknolojia kwenye hatua za kuboresha kilimo ili kuwe na faida kwa wananchi na kuwa na mbegu ambazo zitakuwa vumilivu," alisema.


Naibu makamu mkuu wa Chuo kikuu Cha Sokoine Cha kilimo(SUA) upande wa Utawala, Fedha na Mipango Profesa Amandus Muhairwa, alisema jukwaa hilo linawapa nafasi kwa watanzania kujifunza kutoka kwa wajapani kuhusu uhandisi katika kilimo.

Prof Muhairwa alisema kwa Sasa vijiji vinabadilika kuwa miji hivyo sehemu ndogo ya ardhi inatakiwa kuzalisha zaidi na kuleta tija na hiyo si katika kilimo tu bali hata katika ufugaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI