Header Ads Widget

WATANZANIA TUNA WAJIBU WA KULINDA NCHI NA RASILIMALI ZAKE-WAZIRI KATAMBI


Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Mhe. Patrobas Katambi amesisitiza na kuwakumbusha Watanzania kuwa wanawajibika katika kulinda nchi na rasilimali za Tanzania pamoja na kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia salama na yenye amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii na kila Mtanzania.

Waziri Katambi amebainisha hayo Mkoani Tanga wakati wa muendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akisisitiza kuwa bila amani na usalama hakuna shughuli yoyote ya kijamii ama kiuchumi inayoweza kuendelea.

"Niwakumbushe Watanzania wenzangu kwamba sisi wote Watanzania tunao wajibu wa kuilinda nchi yetu. Jukumu la ulinzi na usalama wa rasilimali, raia wote ni wajibu wetu sote. Haya yote hayawezekani pia kama hakuna usalama kwani kupoteza usalama maana yake hakuna ulinzi, hakuna amani na kama hakuna amani hakuna shughuli  yoyote inayoweza kuendelea."

"Leo tupo hapa tuna amani kwasababu hakuna hata mmoja aliyepigiwa simu na kuambiwa nyumbani kwake wamevamia majambazi, hakuna aliyepigiwa simu na kuambiwa kuwa kuna vurugu mahali na hii ni kwasababu vyombo vyetu vimejidhatiti kiutaalamu na kiteknolojia kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama." Ameongeza kusema Waziri Katambi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI