Header Ads Widget

MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA WAPITISHA BAJETI YA SH, BIL 143

 

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA.

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la mwanza wamepitisha bajeti ya sh Bilioni 143 kwa mwaka wa fedha 2026- 2027 kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo.


 Akisoma bajeti hiyo katika kikao cha Baraza la madiwani cha kujadili na kuidhinisha bajeti ya mwaka wa fedha 2026-2027 kilichofanika Jana oktoba 16, 2026 Mchumi wa halmashauri ya Jiji la mwanza, Jeremia Lubeleje ameeleza vipaumbele 8 vitakavyotekelezwa na halmashauri hiyo.


Akifafanua vipaumbele hivyo ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la mwanza imedhamilia kutekeleza vipaumbele vyake kwa kuboresha miundo mbinu ya Barabara kwa kutenga asimilia 10 ya mapato ya ndani, kuimalisha na kuboresha miundo mbinu ya elimu msingi na sekondari kwa kujenga madarasa nakuongeza madawati kwa ajili ya kupunguza uhaba na sanjari na kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuboresha hali ya lishe na ukamilishaji wa miundombinu ya afya.


Kujenga kitega uchumi cha kisasa cha maduka na maegesho ya magari, kuwezesha shughuri za wananchi za kujiongezea kipato kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kutenga 10% ya mapato ya ndani, kuandaa maandika ya miradi ya kimkakati kwa ajili ya kuongeza mapato, kuimalisha shughuli za upimaji wa makazi na kutoa fidia za ardhi pamoja na kuimalisha sekta ya Sanaa na michezo.


Kwa upande wake meneja Tarura Wilaya ya Nyamagana Mkoani mwanza, Mhandisi Danstan kishaka ameleza kuwa wamepeleka bajeti ya makisio kwa mwaka fedha 2026-2027 kiasi cha Bilioni 6.9 ambazo zitasaidia kutengeneza Barabara za rami takribani kilometa 2, Barbara za zege kilometa 1.9, Barbara za mawe kilometa 2 pamoja na madaraja madogomadogo.


Meya wa Halmashauri ya Jiji la mwanza sima Constantine ameeleza kuwa upitishaii wa bajeti hiyo ni mwanzo wa utekelezaji wa majukumu na kuwataka madiwani kuhakikisha wanawatumikia wananchi ipasavyo.


Naye, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana John Nzilanyingi amemtaka Mkurungenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanatumia nguvu kubwa katika ukusanyaji wa mapato na kuwa na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaonesha ufanisi katika kazi ambazo kwa mwaka 2026-2027 zinazoweza kufanyika. na kueleza kuwa ili bajeti hiyo ifanikiwe ni lazima kuwe na makusanyo ya kutosha.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI