Header Ads Widget

PATUTA YASHIRIKI MAPOKEZI YA MAKAMU WA RAIS RUVUMA


TAASISI ya Pamoja Tutashinda Tanzania (PATUTA ORGANIZATION) imeshiriki katika mapokezi rasmi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye amewasili Songea, Mkoani Ruvuma kushiriki tamasha la kumbukizi ya miaka 120 ya mashujaa wa vita ya Majimaji.

Katika mapokezi hayo, PATUTA Organization imeongozwa na Mkurugenzi wake, Dkt Aiden Ndaombwa pamoja na Naibu Katibu wa taasisi hiyo, Wencyslaus Kaashindye na Machifu wa kutoka Songea, Lindi, Mtwara na Arusha ambao kwa pamoja waliungana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta binafsi,

Aidha upande wa viongozi wa Serikali, Dkt. Nchimbi amepokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiambata na Mkurugenzi wa Idara ya Malikale Dkt. Christowaja Ntandu, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, viongozi na Wananchi wa mkoa huo. 

Februari 27 ya kila Mwaka Tanzania huadhimisha Maadhisho hayo kwa matukio mbalimbali kama sehemu ya kuenzi na kuthamini mchango wa wapigania ukombozi wa Taifa la Tanganyika kwa sasa Tanzania ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni:

"Utamaduni Wetu Ndiyo Nguvu Yetu kwa Maendeleo ya Utalii na Uchumi Wetu''








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI