Header Ads Widget

SERIKALI YA RAIS SAMIA YATANGAZA KUNUNUA NDEGE MPYA NANE KWA MWAKA HUU



Msemaji Mkuu wa serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa leo Alhamisi Februari 26, 2026 amewaambia waandishi wa habari Mjini Dar Es Salaam kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa mwaka huu imepanga kununua ndege mpya nne kati ya nane walizopanga kununua ili kuongeza fursa kwa watanzania katika masoko ya kikanda na Kimataifa pamoja na kusisimua uchumi na Utalii wa Tanzania kama ilivyoahidiwa katika Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Dar Es Salaam, Msigwa amesema  ndege zitakazonunuliwa ni aina ya Bombardier Q400 kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa serikali katika kuimarisha mtandao wa huduma za usafiri wa anga ili kuwa kichocheo muhimu cha Utalii, biashara na usafiri.

"Mimi nipo hapa kuwahakikishia kwamba katika lengo hili tumepata mafanikio makubwa, shirika letu sasa hivi tumepata mafanikio makubwa ambapo tumeanza kutajwa kama Shirika lenye nguvu zaidi barani Afrika katika mtandao wake na sasa tunayoa huduma katika vituo zaidi ya 33 ndani na nje ya nchi kwa kutumia ndege zetu 16 tulizo nazo sasa." Amesema Bw.  Msigwa.

Katika ndege hizo zilizokabidhiwa kwa Shirika la ndege, Msigwa amesema ndege nne zinafanya safari ya masafa marefu kwenda Mumbai, Johannesburg na Accra huku ndege nyingine zikifanya masafa ya kati na mafupi, mpango sasa ukiwa ni kuelekea Pemba, Lagos, Kinshasa na Cape Town, lengo likiwa ni kuongeza fursa na uhakika wa usafiri na fursa za biashara na mapato ya kigeni.

Msigwa katika hatua nyingine amesema serikali pia inaendelea kuwekeza katika ununuzi wa ndege mpya ili kuboresha shirika hilo lakini pia kuboresha karakana, kuimarisha mazingira ya kazi na kuboresha huduma zinazotolewa katika Viwanja vya ndege hapa nchini.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI