Header Ads Widget

CPA MUSA KUJI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA BAJETI YA SHIRIKA KWA MWAKA WA FEDHA 2027/2027

 


Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) CPA Musa Nassoro Kuji, leo Februari 13, 2026 ameongoza kikao cha Kamati ya Bajeti ya Shirika kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi Kiunganishi ya TANAPA iliyopo Jijini Dodoma.

Kikao hicho kililenga kupitia mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti, ikiwa ni pamoja na mapitio ya Mpango Mkakati wa Shirika 2026/2027–2030/2031, malengo, mikakati, na mbinu za utekelezaji.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wanakamati wa kamati hiyo pamoja na timu ya menejimenti ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa pamoja ili kuchangia katika kujenga mwongozo madhubuti wa bajeti na mikakati ya Shirika katika kufanikisha lengo la taasisi na Taifa kwa ujumla kwa kuimarisha uhifadhi ndani ya Hifadhi za Taifa pamoja na kuboresha shughuli za utalii ili kuongeza pato la Taifa.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI