![]() |
| Jenerali Davis Mwamunyange. |
DAR ES SALAAM: TUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, Leo Februari 13 imekutana na Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Jenerali George Waitara na Jenerali Davis Mwamunyange.
Mahojiano hayo ya Tume na Wakuu hao wastaafu yamefanyika kwa nyakati tofauti katika Ofisi za Tume hiyo zilizopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na namna Matukio haya yalivyoanza, yalivyoathiri wakazi wa Mkoa wa Arusha, Mali na Miundombinu yake.
Hata hivyo Tume inaendelea na mahojiano na waathirika wa Matukio hayo kwa ajili ya hatua zaidi kama Taifa ili Matukio kama hayo yasijirudie tena.
![]() |
| Jenerali George Waitara |












0 Comments